Home | Terms & Conditions | Help

November 23, 2024, 5:32 pm

News: Mwakyembe amwiekea Kauzibe Tundu Lissu kwenye chama cha wanasheria

Dodoma: Zikiwa zimebaki siku chache za kufanyika kwa uchaguzi wa chama cha wanasheria Tanganyika, Tanganyika Law of Associate(TLS). Waziri wa mambo ya Sheria na katiba Dr Harrison Mwakyembe amepinga vikali kuingia kwa Siasa kwenye chama hicho na kusema kuwa yupo tayari kukivunja pale itapobidi, Kauli hiyo ameitoa Jana mjini Dodoma pale abapo alipo tembelewa na Wanasheria wa chama hicho akiwemo Rais wa chama hicho Ndugu John Seka.

Mwakyembe alisema "Kama wizara hatujui mwelekeo wa TLS kwa sasa, hatuwezi kuiacha TLS ikijiingiza katika siasa halafu tukawaangalia tu. Hatuna nia ya kuitawala TLS, ila tunawajibika kuwasimamia kwa kuwa Sheria yenu iko chini yetu, mkiharibu kwa lolote wizara ndio yenye wajibu wa kuwatolea maelezo katika hilo mnalotaka kulifanya sasa kuna mgongano wa maslahi, je, ninyi kama wanasheria hamkuliona au hamlioni?” Alihoji Mwakyembe.

Wagombea wa TLS Mmoja wa wanasiasa wanaowania urais wa TLS ni Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu ambaye juzi alisema kitendo cha kukamatwa baada ya kufutiwa kesi, kina nia ya kufifisha harakati zake za kuwania urais wa TLS wiki ijayo, huku akitishia kugoma kula, endapo hatapelekwa mahakamani mapema.

Lissu ambaye ni mbunge kwa tiketi ya Chadema, alikuwa na kesi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, akituhumiwa kutumia lugha ya uchochezi katika kampeni za uchaguzi Jimbo la Dimani, Zanzibar.

Mbali na Lissu, wagombea wengine wanaowania nafasi hiyo inayoshikiliwa na Rais wa sasa, John Seka ni kada wa Chadema, Lawrence Masha na aliyewahi kuwa rais wa chama hicho mwaka 2011 hadi 2013, Francis Stolla.

Wengine ni Godwin Mwapongo na Victoria Mandari. Uchaguzi wa chama hicho unatarajia kufanyika Machi 18, mwaka huu na mawakili 6,000 watapiga kura kumchagua Rais mpya wa TLS.

Pia Tarehe za nyuma kidongo Mhadhiri wa chukikuu Cha Dar es salaam Prof. MKUMBO aliandika kuwa Mwakyembe amewasaidia wajumbe wa TLS Kumjua Tundu Lissu