- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MVUA KUBWA KUENDELEA KUITESA DAR MPAKA MEI 17
Dar es Salaam: Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA) imetoa tahadhari Jana Mei 13 ya kunyesha mvua kubwa kwa siku tano, ambazo zinaweza kuleta mafuriko katika maeneo ya mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani, Lindi, Mtwara na Visiwa vya Unguja na Pemba.
Katika taarifa ya TMA, inasema mvua hizo zilizoanza kunyesha jana , zitaendelea mpaka Mei 17 mwaka huu.
TMA imesema kuwa athari za mvua hizo ni pamoja na kutokea kwa mafuriko yatakayo sababisha barabara kuto pitika, watu kuhama kwenye makazi yao, hivyo kusababisha maisha ya watu kuwa hatarini kutokana na maji kujaa au kupita kwa kasi. Pia imetoa wito kwa wakazi wa maeneo hayo kuchukua tahadhari stahiki na kuendelea kufuatilia taarifa pamoja na tahadhari zitakazotolewa.