Home | Terms & Conditions | Help

November 30, 2024, 2:49 am

NEWS : MUUNGANO WA KIJESHI WA MAREKANI WAKIRI KUUWA RAIA NCHINI IRAQ

Muungano wa kijeshi wa Marekani wakiri kuua raia 892 wa Syria na Iraq

Muungano wa kijeshi wa Marekani wakiri kuua raia 892 wa Syria na Iraq

Muungano wa kimataifa unaoongozwa na Marekani wa eti kupambana na kundi la kigaidi na ukufurishaji la Daesh (ISIS) umekiri kupitia ripoti uliyotoa hapo jana kuwa tangu yalipoanza mashambulio ya anga ya muungano huo mwaka 2014 hadi sasa raia 892 wameuawa katika nchi za Syria na Iraq.

Katika ripoti iliyotolewa na muungano huo mwezi Aprili, ilielezwa kuwa raia 883 wameuawa katika nchi za Syria na Iraq kutokana na mashambulio yaliyofanywa na muungano huo unaojiita wa kimataifa wa kupambana na Daesh.

Hata hivyo ripoti za kuaminika zinaonyesha kuwa zaidi ya raia elfu tatu wameuliwa katika nchi hizo mbili za Kiarabu katika mashambulio ya anga yaliyofanywa na muungano wa kijeshi unaoongozwa na Marekani kwa kisingizio cha kutokomeza ngome za kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh.

Tangu mwezi Agosti mwaka 2014 hadi sasa, muungano huo wa kijeshi unaoongozwa na Marekani umeshafanya mashambulio ya anga zaidi ya 29,000 ndani ya ardhi za Syria na Iraq.

Maiti ya kitoto kilichotolewa kwenye kifusi baada ya shambulio la muungano wa kijeshi unaoongozwa na Marekani nchini Syria

Serikali ya Syria imemwandikia barua mara kadhaa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na rais wa Baraza la Usalama la umoja huo kutaka jinai zinazofanywa nchini humo na muungano wa kijeshi unaoongozwa na Marekani zikomeshwe.

Muungano eti wa kupambana na Daesh ulianzishwa na Marekani wakati wa urais wa Barack Obama kwa madai ya kupambana na magaidi walioko katika nchi za Syria na Iraq. Hata hivyo ripoti rasmi zinaonyesha kuwa Marekani yenyewe pamoja na washirika wake wa Magharibi na baadhi ya nchi za Kiarabu ni miongoni mwa waanzilishi na wafadhili wakuu wa fedha na silaha kwa makundi hayo ya kigaidi likiwemo la Daesh (ISIS)