- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MTOTO WA RAIS ZUMA AFIKISHWA MAHAKAMANI
Mtoto wa Rais mstaafu wa Afrika Kusini Jacob Zuma, Duduzane Zuma amefikishwa mahakamani, ambayo ni mahakama maalum inayoshughulikia kesi za rushwa huko Johannesburg.
Duduzane Alifikishwa mahakamani Jana jumatatu, huku miguu yake ikiwa imefungwa mnyororo.
Zuma ameachiliwa baada ya kulipa dhamana ya rand 100,000.
Mamlaka imemnyang'anya pasipoti yake.
Mahakama imeahirisha kesi ya mtoto huyo wa Jacob Zuma hadi Januari 24 kwa ajilia ya uchunguzi zaidi.
Tangu baba yake kutimuliwa mamlakani, ni mara ya kwanza vyombo vya shera vya Afrika Kusini kushughulikia kesi yamtoto wa Jacob Zuma anayeshtumiwa kuhusika katika kesi kadhaa.
Duduzane Zuma, ambaye alirejea Afrika Kusini siku ya Ijumaa kuhudhuria mazishi ya mmoja wa ndugu zake, aliwekwa kizuizini kwa masaa kadhaa na polisi katika uwanja wa ndege wa Johannesburg.
Wiki ijayo atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili katika kesi nyingine ya mauaji wakati wa ajali ya gari mwaka 2014 ambapo alimuua mwanamke mmoja na kumjeruhi mtu mwingine ambaye alifariki dunia baadaye. hospitalini.
Hata hivyo Duduzane Zuma amefutilia mbali tuhuma dhidi yake katika ajali hiy