Home | Terms & Conditions | Help

November 30, 2024, 7:33 pm

NEWS: MSINGWA AWAOMBA RADHI WANACHADEMA KWA KUMSIFIA RAIS MAGUFULI

Iringa: Mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa amewaomba Radhi wanachama wote wa chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema na wafuasi wa Mbunge huyo kwa kile kinachojulikana kuwa alimsifia na kupongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli kwa maendeleo wakati wa warsha ya ufunguzi wa barabara ya Iyovi – Iringa – Mafinga yenye urefu wa kilometa 218.6 hivyo kuzusha sintofahamu kwa wanachama wa chama hicho na wafuasi wa mbunge huyo wa Iringa.

Akiongea kupitia Ukurasa wake wa Twitter Jana May 3 Msigwa aliwaomba radhi baada ya kugundua kuwa wanachama hao na marafiki zake hawakumuelewa kwenye ufafuzi wa awali baada ya kuongea maneno yale mele ya rais Magufuli ''Ufafanuzi wangu bado haueleweki na ni heshima kuzingatia maumivu yenu kwa mkanganyiko huu. Nagundua rafiki zangu na wanachama wetu wanaugua. Basi niseme nini?Naomba nisameheni sana. The cause we are fighting for is more important than my personality. I take full responsibility" alisema Msigwa

Msigwa alipata nafasi ya kuongea kwa niaba ya wana iringa mjini kwenye warsha ya ufunguzi wa barabara ya Iyovi – Iringa May 2 nakuonekana kutoa maneno ya pongezi kwa Rais magufuli kwa kuleta maendeo katika jimbo lake

"Mh. Rais umekuwa ukisisitiza katika hutuba zako kwamba wewe hujali vyama, na hili limedhihirika kwakweli hujali vyama, umesaidia sana, kwa bahati mbaya haukupangiwa Ratiba ya kufungua miradi, hela za kutoka kwako zimekuja nyingi, amezungumza Mh. Mahinga tunabarabara nzuri katika kipindi chako umekuwa Rais, Tumejenga barabara ya lami mradi wa World Bank kutoka mlandege mpaka kwa mkuu wa wilaya karibu Bilioni 3.5. tunastendi nzuri ipo hapo ipogolo karibu bilioni 3 , tuna maji kwahiyo kunavitu vimefanyika kwakeli Mh. Rais Hupendelei hata sisi Wachadema huwa unaleta hela, kwahilo nikupongeze sana" alionge Msigwa mbele ya Rais Magufuli

Baada ya maneno hayo ndipo mijadala ikazuka kwenye mitandao ya kijamii na kuanza kuleta taharuki na majibizano kati ya wanachama wa chadema na wale waccm ndipo Msigwa akatolea ufafanuzi dhidi ya wale wanaosema kuwa alimsifia Rais Magufuli na Serekali yake

"Vijana wa ccm wanatamani sana nionyeshe naiunga mkono serikali ya awamu ya tano! (Dying for my endorsement ) Mtasubiri sana" alisema msigwa

Rais Magufuli tarehe 02 Mei, 2018 ameweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Kilolo Mkoani Iringa na kuwahakikishia wananchi wa Wilaya hiyo kuwa Serikali itahakikisha ujenzi wa hospitali hiyo unakamilika haraka na kupeleka madaktari na wauguzi kwa ajili ya kuanza kutoa huduma.

Majengo ambayo yameanza kujengwa ni jengo la matibabu kwa wagonjwa wa nje (OPD), jengo la mionzi (Radiology), jengo la huduma ya mama na mtoto (RCH), jengo la maabara na jengo la wodi za kulaza wagonjwa, ambapo tayari Serikali imetoa Shilingi Bilioni 4.2 na hospitali inatarajiwa kuanza kutoa huduma ifikapo mwezi Agosti 2018.