- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MSIMAMO WA CHADEMA KUHUSU MGOMBEA URAIS ALIYEJITANGAZA
Dar es salaam. Chama kikuu cha Upinzani nchini Tanzania CHADEMA kimesema kuwa mpaka hivi sasa hakuna tangazo lolote la chama lililotoka ambalo, linawapa nafasi watangaza nia kwa nafasi ya kugombea Urais na Ubunge ndani ya chama hicho, wala kuwasilisha taarifa zao kwa Katibu Mkuu wa chama hicho.
Kauli hiyo ya Chama imetolewa leo Mei 26, 2020 na Mkuu wa Idara ya Mawasiliano wa chama hicho, Tumaini Makene wakati akifanyiwa mahojiano na Kituo cha Habari cha East Africa Redio Jijini Dar es salaam na kuongeza kuwa kwa mwanachama yeyote wa chama hicho, hata kabla ya kutangaza nia ya kugombea ni lazima atakuwa ameisoma na kuilewa katiba ya CHADEMA.
Kauli hiyo ya Makeni imejiri kufuatia mwanamama ambaye ni mwanachama wa Chadema Dkt Mayrose Majinge, kutangaza nia ya kugombea nafasi ya Urais kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika uchaguzi mkuu unaokusudiwa Octoba mwaka huu.
"Lakini kabla ya kuwasilisha, katika sehemu ambayo unakuwepo kunakuwa na tangazo limetoka na watu wanapeleka makusudio yao ofisi ya Katibu Mkuu, halafu process zingine zinafuata kwa mujibu wa chama, na tangazo la watu kuwasilisha nia zao bado halijatoka"amesema Tumaini Makene.
Pia Makene ameongeza kuwa,"Tunaamini kwamba kwa mtu yeyote ambaye ni mwana CHADEMA, anafahamu utaratibu kabla ya kutangaza nia ya nafasi hiyo kubwa kwamba atakuwa amesoma Katiba ya chama, kwahiyo tunaamini kwamba hakuna mtu atakayekiuka utaratibu huo".