- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MSIGWA AMUUNGA MKONO WAZIRI LUGOLA SWALA LA MABASI KUSAFIRI USIKU
Mbunge wa Iringa mjini (Chadema) Mchungaji Peter Msigwa ameunga mkono kauli ya Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Kange Lugola juu ya swala la mabasi kusafiri usiku na watu kufanya kazi saa 24.
Akiongea Leo July 19 Kupitia ukurasa wake wa twitter Msigwa amesema Kuwa anaunga mkono swala la mabasi kutembea usiku kwa sababu nchi za kusini mwa Africa na Africa mashariki pia mabasi yanatembea usiku kwanini na sisi tusitembee usiku.
" Mabasi kutembea usiku namuunga mkono Waziri Kangi.Nakumbuka amri ya mabasi kuto kusafiri usiku ilitolewa na Malecela akiwa Waziri Mkuu wakati huo baadaya ajaili mbaya ya basi la super star na kuua watu wengi! Karibu nchi zote za Kusini na afrika mashariki mabasi yanasafiri usiku"
July 17, 2018 Lugola, alitoa muda wa siku 14 kwa Inspekta Jenerali wa Polisi, IGP Simon Sirro kufika ofisini kwake kumueleza mikakati ya kuwawezesha Watanzania kufanya kazi kwa saa 24 ikiwa ni pamoja na kuzuia matishio ya mabasi kutembea nyakati za usiku.
Waziri Lugola alitoa agizo hilo mara baada ya kufanya ziara ya kikazi katika makao makuu ya kikosi cha kutuliza ghasia kilichopo Ukonga Jijini Dar es Salaam na kuongea na Askari wa Kikosi hicho na wale wanaohudumia katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere.
Wakati akitoa agizo hilo, Mhe. Lugola alisema kuwa ili kufikia Uchumi wa kati Watanzania wanatakiwa kufanya kazi za kiuchumi kwa masaa 24 hivyo IGP anapaswa kumhakikishia mikakati ya jeshi lake katika ushiriki wao wa kuwapatia watanzania usalama kwa muda wote wakifanya shughuli hizo za kiuchumi.
"Nataka IGP aje aniambie kwamba je, jeshi la polisi limesalimu amri kwa majambazi ndiyo maana mabasi hayatembei usiku, lakini biashara mbalimbali ikifika saa 12 zinafungwa, ukiuliza unaambiwa ni kwa sababu ya usalama, nataka IGP aniambie kama majambazi ndio wanaotupatia amri...Hatuwezi kukubali kupewa amri na majambazi ni masaa mangapi tunatakiwa kufanya shughuli za kiuchumi au kupangiwa maeneo ya kwenda na wapi tusiende,"Waziri Lugola.