- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
News: Mshauri wa Rais Donald Trump ajiuzulu
Washington: Mshauri mkuu wa rais Donald Trump amejiuzulu baada ya kukabiliwa na kushfa ya udanganyifu, kuhusiana na mazungumzo aliyoyafanya na balozi wa Urusi. Ikulu ya White House imekwishatangaza atakayekaimu katika nafasi hiyo.
Mshauri huyo, Michael Flynn hapo awali alikuwa amekanusha kuhusisha suala la vikwazo dhidi ya Urusi, katika mazungumzo na balozi wa Urusi nchini Marekani Sergei Kislyak, wakati ambapo alikuwa hajaanza rasmi majukumu yake.
Hili linachukuliwa kama pigo kubwa kwa utawala wa Donald Trump ambao haujadumu hata kwa kipindi cha mwezi mmoja. Kwa siku kadhaa uvumi umekuwa ukienea, kwamba Flynn ambaye ni Jenerali mstaafu, alimdanganya Makamu Rais Mike Pence, ambaye alijitokeza hadharani kumtetea.
Katika barua yake ya kujiuzulu, Flynn amesema ''bila kukusudia'' alimpa Makamu Rais ''taarifa ambazo sio kamilifu'' kuhusu mazungumzo yake ya simu na balozi Kislyak wa Urusi.
Ikulu ya White House mjini Washington imesema imemteuwa Luteni Jenerali Joseph Kellogg ambaye amekuwa mwenyekiti wa baraza la majenerali, kukaimu katika nafasi iliyoachwa wazi na Michael Flynn. Vyombo vya habari nchini Marekani viliripoti jana Jumatatu, kwamba utawala wa Donald Trump ulikwishatahadharishwa mapema mwaka huu kuhusu mahusiano kati ya Michael Flynn na Urusi.