- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MSANII WA INJILI KENYA ATAKA KUMUOA ZARI ILI AMTUMIKIA MUNGU
NAIROBI: Msanii wa muziki wa Injili tokea nchini Kenya Alex Apoko ,maarufu Ringtone ameonyesha hamu na Shauku ya kutaka kumchumbia Mzazi mwenza wa Msanii maarufu wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Zari Hassani ambaye ni mama wa watoto watano.
Ringtone anayejulikana kwa wimbo wake 'Tenda Wema' aliyeimba na msanii wa Tanzania Christine Shusho anasema kuwa yeye ndio suluhu kwa matatizo ya kimapenzi ambayo yamekuwa yakimzonga mfanyibiashara huyo wa Uganda.
Msanii huyo sasa amemtaka mfanyibiashara huyo kutokubali kumrudia Diamond Platinumz na badala yake kukubali uchumba wake kwa lengo la kumtumikia Mungu.
''Diamond aniwachie Zari, Zari ni wangu wa Moyoni, atuwache tumtumikie Mungu'', alisema Ringtone alipohojiwa na chombo cha habari cha BBC mjini Nairobi.
Msanii huyo anasema kwamba aliota ndoto siku ambayo wawili hao waliachana ambapo anadai kumuona Zari.
''Nilipoamka nikahisi moyo wangu unamtaka mwanamke huyu na sio mtu mwengine yeyote, hapo nilijiuliza maswali na nikasikia sauti upande mwengine ikiniambia usijali kile watu watakachozungumza fuata Moyo wako na usimkosee Mungu''.
Alipoulizwa kwa nini unamtaka Zari, Ringtone alikua mwepesi wa kujibu akisema kuwa ni mwanamke mrembo na mpenda biashara.
Anasema kwamba kwa kuwa amepiga hatua katika safu ya muziki anadhani kwamba Zari atamsaidia pakubwa kuendeleza biashara zake iwapo watafunga ndoa.
Vilevile amesema kuwa mfanyibiashara huyo wa Uganda ambaye kwa sasa amekita kambi nchini Afrika Kusini hafai kuumizwa na kuvunjwa moyo mara kwa mara.
''Zari Hassan anahitaji mwanamume ambaye atampenda kwa moyo wake wote na kumpeleka kanisani. Diamond hawezi Kufanya hivyo''.