- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MSAMI NA RAIS WA MDUARA AT WAINGIA KWENYE BIFU
Dar es salaam: Msanii anye iwakilisha bongo fleva na mtaaalam wa kufanya choreograph hapa nchini Msami baby, amefunguka baada ya kile kinachoelezwa ni kauli ya dharau na kukera iliyosemwa na mkongwe wa muziki ambaye ni mkali wa miondoko ya mduara, A.T.
Awali AT alinukuliwa akisema "si wasanii wabovu tu wanaopewa promotion kama alivyosema Tundaman bali hata madensa pia". Kauli hii imemkera msami na kupelekea kutokwa na maneno au povu dhidi ya mkongwe huyo. Msami alisema kuna wasanii wengi wanaojua kuimba na wenye mashabiki wengi kupita yeye, hivyo mtu asimdharau msani mwingine kwani mungu ndiye humpangia mtu mafanikio,
Akitolea mfano wake yeye na kundi la makomando ni baadhi ya wasanii wenye asili ya kudensi japo wanafanya vizuri katika muziki huu. Alisisitiza kuwa "kudensi ni ajira na watu wanaishi kwa kazi hiyo na isiwe sababu ya kumdharau mwingine kwani hata AT amekwisha mpigia simu mara kadhaa kuomba madensa wa kutumbuiza katika matamasha yake"