- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
News: Msako wa Viroba chini Wamuwa Mfanyabiashara moja Mkoani Dodoma
Dodoma; Mfanyabiashara maarufu wa viroba Festo Mselia mkaazi mkoa wa Dodoma , anaye daiwa kujiuwa kwa risasi baada ya kukanguliwa mara mbili na polisi kutokana na kumiliki bidhaa hiyo ambayo kwa sasa imekuwa ni gumzo hapa nchini kulingana na kampeni ya serekali kuwataka wazalishaji wa huduma hiyo kubadili mfumo vifungashio, kutoka kwenye lailoni mpaka kwenye mfumo wa chupa ngumu.
Kampeni ya kukamata wafanyabiashara wa viroba nchini, inayo simamiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) ilianza Machi mosi mwaka huu, baada ya Serikali kutoa taarifa ya mwisho wa biashara hiyo tangu Mei, mwaka jana. ambapo waziri mwenye zamana hiyo Mh January makamaba alitangaza vita dhida ya wazalishaji wa bidhaa hiyo ichi nzima.
Mei mwaka jana, Serikali ilibainisha kuwa kuanzia kipindi hicho hadi Januari mosi mwaka huu, ungekuwa mwisho wa kuzalisha na biashara ya pombe kali inayohifadhiwa katika vifungashio hivyo (viroba).
Hata hivyo, Januari mwaka huu Serikali iliongeza muda hadi Machi mosi ili kutoa nafasi tena kwa wafanyabiashara waliokuwa na shehena ya vinywaji hivyo waliofuata taratibu, kumaliza, lakini wengi wamekamatwa wakiwa nazo katika msako unaoendelea hivi sasa.
Mfanyabiashara huyo anayemiliki kampuni ya Mselia Enterprises na duka la bia za jumla, baa na nyumba za kulala wageni mjini Dodoma, alijipiga risasi kwenye shavu la kushoto juzi, Jumanne akiwa shambani kwake Veyula, nje kidogo ya mji wa Dodoma.
Daktari wa zamu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, Carolyn Damian alisema alimpokea Mselia hospitalini hapo akiwa mahututi saa 7 usiku, na kumweka katika chumba cha uangalizi maalumu (ICU) na robo saa baadaye alifariki.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Lazaro Mambosasa alithibitisha kupewa taarifa na mtu kuhusu kusikika kwa mlio wa risasi saa 3 usiku na baadaye saa 5 aliwatuma askari na kwenda kuchunguza na ndipo walipomwona mfanyabiashara huyo, amejipiga risasi na alikufa kutokana na kutokwa na damu nyingi.
Mambosasa alisema baada ya kupewa taarifa, askari walifuatilia eneo ambalo risasi zilisikika katika shamba la mfanyabiashara huyo eneo la Veyula na walipofika, waliokota maganda matano ya risasi alizotumia kujiua.
Mfanyakazi wa mfanyabiashara huyo, Leslie Msigwa alisema ni kweli polisi walikwenda mara mbili dukani kwake Barabara ya 11, karibu na Ofisi za TFDA, na mara ya mwisho waliondoka naye akiwa kwenye gari lake prado likiendeshwa na mteja wao, Mazengo hadi waliposikia kwamba amejiua shambani kwake, Veyula Dodoma.
Msigwa alisema ni kweli kwenye stoo yake, kulikuwa na katoni 1,269 za viroba pamoja na vinywaji vingine, ambavyo huwa wanasambaza katika baa na maduka mbalimbali.