Home | Terms & Conditions | Help

November 23, 2024, 11:11 pm

News: Mkuu wa wilaya ya Dodoma asisitiza kila mtanzania kuwa na kitambulisho cha Uraia.

Dodoma: Zoezi la usajili wa vitambulisho vya taifa limezinduliwa rasmi katika wilaya ya Dodoma mjini, ambapo jumla ya watumishi elfu 7682 wamepatiwa vitambulisho hivyo ikiwa lengo ni kuwafikia watumishi elfu 8283 na wanachi zaidi ya laki nne watapatiwa vitambulisho hivyo.

Katika uzinduzi huo mkuu wa wilaya ya dodoma mjini Christina mndeme amewata watumishi wa serikali pamoja na wananchi kuhakikisha wanafichua watu wasiostahili kupewa vitambulisho vya uraia. Zoezi la usajili wa vitambulisho vya taifa kwa watanzania limeendelea kufanyika lengo likiwa ni kila mtanzania kupatiwa kitambulisho chake cha uraia jambo litakaloisaidia serikali kuwatambua wananchi wake na kuondoa wa mwingiliano wa watu wasio raia wanaoishi kinyume cha utaratibu wa sheria za nchi.

Kupitia uzinduzi huo mkuu wa wilaya CHRISTINE MNDEME anatoa angalizo kwa wananchi. pamoja na maelekezo kwa mamlaka ya vitambulisho vya taifa NIDA kuhakikisha wanaongeza juhudi katika zoezi hili la kutoa vitambulisho vya taifa.

Mkuu wa wilaya amesisitiza umuhimu wa kila mwtanzania kupata kitambulisho cha taifa.. Zoezi hilo la utambuzi wa watumishi wa serikali lilianza octoba 3- 2016 katika wilaya ya Dodoma mjini ambapo lilianza kwa watumishi wa serikali na sasa limeanza kwa Kata ya Kilimani na Tambuka Reli katika Manispaa ya Dodoma.