- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
News: Mkuu wa mkoa wa Dodoma awataka wafanyabiashara kutopandisha bei ya bidhaa
Dodoma: Wafanyabiashara katika mkoa wa Dodoma wametakiwa kutopandisha bei ya bidhaa zao kwa kutumia kigezo cha dodoma kuwa makao makuu na ujio wa sherehe mbalimbali za kitaifa badala yake wanatakiwa kuboresha biashara zao.
Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana,wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya kufanyika kwa sherehe Muhungano ambazo zitafanyika kitaifa mjini hapa.
Mkuu huyo amesema licha ya wafanyabiashara kutakiwa kutumia fursa ya ujio wa makao makuu pamoja na kufanyika kwa shughuli mbalimbali za kitaifa lakini haina maana yoyote kwa wafanya biashara hao kupandisha bei za bidhaa.
“Najuaa kitendo cha Dodoma kuwa makao makuu kinawafanya wafanyabiashara kupata fursa ya kujiongezea kipato, lakini jambo kubwa zaidi si kupandisha bei za bidhaa bali ni kuhakikisha bidhaa zinaboreshwa ili kuhakikisha ushindani wa kibiashara unakuwa mzuri kwa wale wanaopata huduma” alisema Rugimbana.
Akizungumzia kuhusu sherehe za Muungano kufanyika mkoani hapa amesema wananchi wa mkoa wa Dodoma wasiwe na hofu kutokana na kuwepo kwa viongozi wengi hasa wanajeshi wa jeshi la kujenga taifa,amesemann wapo katika kufanyika kwa mazoezi juu.
“Wananchi naomba kuwatoahofu kuwa kwa sasa mji wa Dodoma, kuna wageni wengi pia wapo wanajeshi wengi pamoja na vifaa mbalimbali kama vile vifaru na ndege za kivita ambapo wanajeshi hao wanafanya mazoezi.
“Pamoja na kuwepo kwa ugeni huo wananchi wanatakiwa kujipanga kwa ajili ya kuwakaribisha wageni mbalimbali sambamba na kuboresha mazingira ya kibiashara huku wakijiandaa kwa lengo la kupokea sherehe hizo” alisema Rugimbana.