- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MKUU WA MKOA APINGA MAAGIZO YA MKEMIA MKUU WA SEREKALI
BABATI: Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti amekifungua kwa lazima kiwanda cha pombe kali cha Mati Super Brand kilichofungwa na Mkemia Mkuu wa Serikali kilichopo mjini Babati mkoani Manyara na kutaka akamatwe yeye, badala ya wamiliki wa kiwanda hicho.
Mnyeti amefanya maamuzi hayo leo Juni 23, 2018 kwa maelezo kuwa hakubaliani na sababu zilizotolewa mpaka kiwanda hicho kufungwa Machi, 2018.
Mkemia Mkuu wa Serikali alikifunga kiwanda hicho kwa maelezo kuwa kimekosa kibali cha kuidhinisha matumizi ya kemikali za kuzalisha pombe hizo.
Amesema mwekezaji huyo amefunga mitambo yake na kutoa ajira kwa wananchi, badala ya kupewa ushirikiano watendaji wanaohusika wanamkwamisha kwa kukifunga kiwanda, ikiwa ni takribani miezi mitatu sasa. "Bado kuna watu wamelala wanaandaa mazingira ya rushwa, yaani badala watumie hata siku tatu za kumshauri kitaalamu wanakimbilia kufunga kiwanda," amesema Mnyeti.
“Kuna baadhi ya watumishi wa Serikali wana ukiritimba mno, sasa mimi nakifungua kiwanda hiki halafu wakija wanikamate mimi," amesema.
Amesisitiza kuwa katika Kata ya Terrat WIlaya ya Simanjiro kuna kiwanda cha kusindika nyama ya ng'ombe ambacho kimefungwa, kwamba nacho atakwenda kukifungua. Awali, Mkurugenzi wa kiwanda hicho, David Mulokozi amesema wakati wa uzalishaji alikuwa analipa zaidi ya Sh100 milioni ya kodi Serikali ila hivi sasa wamesitisha uzalishaji baada ya kiwanda hicho kufungwa.
Mulokozi amesema walifikisha suala hilo kwa Mkuu wa Wilaya ya Babati, mhandisi Raymond Mushi ambaye alitoa agizo suala hilo lishughulikiwe mara moja lakini hakukuwa na utekelezaji.