- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MKUTANO WA ZITTO WAZUÌLIWA NA JESHI LA POLISI
Jeshi la Polisi Kigoma limemzuia Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe kufanya mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Mwanga Community Center, mkoani Kigoma ambao ulipaswa kufanyika leo Januari 16, 2018
Taarifa iliyotolewa na OCD inasema kuwa kiongozi huyo hakufuata utaratibu wa kutoa taarifa ndani ya masaa 48 kabla ya kufanyika kwa mkutano huo jambo ambalo Mbunge Zitto Kabwe amelilamikia nakusema kuwa amezuiwa kufanya Mkutano kinyume na sheria ya Bunge ya mwaka 1988.
"Mimi sitaki kuwapa polisi sifa ya kupambana nasi. Tumeahirisha mkutano mpaka siku ya jumamosi Lakini tumewaandikia barua rasmi kuwa sheria waliyonukuu sio sheria halali na haihusiani na mikutano ya Mbunge kwenye jimbo lake la Uchaguzi. Sheria wanayopaswa kunukuu ni sheria namba 3 ya mwaka 1988 kifungu cha 4(1)". Alisema Zitto Kabwe
Kufuatia jambo hilo Zitto Kabwe amedai kuwa atamwandikia barua rasmi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai kuhusu suala hilo ili kutengeneza mazingira kwa siku za usoni lisije kumtokea Mbunge mwingine yoyote