- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MKURUGENZI KINONDONI KORTINI KWA UBADHIRIFU
Dar es salaam. TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Kinondoni jana imemfikisha mahakamani aliyekuwa Mkurungenzi wa Manispaa ya Kinondoni Mussa Natty na wenzake waliokuwa maofisa wa Manispaa hiyo kwa makosa ya rushwa.
Mbali na Mkurugenizi huyo wengine ni Baraka Mkuya aliyekuwa Mhandisi, Ismail Mafita aliyekuwa mhandisi wa Barabara na Ernest Ngolofu aliyekuwa Mkadiriaji Majenzi.
Akitoa taarifa hiyo jana Mei 18, 2020, Mkuu wa Takukuru Kinondoni, Pilly Mwakasege, alisema watu hao wanashtakiwa kwa kosa la matumizi mabaya ya madaraka kinyume na kifungu cha 31 Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na 11/2007 na kula njama kutenda kosa kinyume cha kifungu 32 cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa Na 11/2007.
“Awali ofisi ya Takukuru ya Mkoa wa Kinondoni ilipokea malalamiko yanayohusu Manispaa ya Kinondoni kuwa kumefanyika ubadhilifu wa fedha katika miradi ya ujenzi wa barabara za Journalism yenye urefu wa 0.53 km, Feza/Senga yenye urefu 0.75 km na Serengeti yenye urefu 0.6 km zilizopo katika manispaa hiyo ikiwa ni pamoja na kumwongezea mkandarasi kazi bila kufuata taratibu za manunuzi,” alisema Mwakasege.
Alisema uchunguzi dhidi ya tuhuma hizo umebaini mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwa Manispaa ya Kinondoni iliingilia mkataba wa Kampuni ya Skol Building Contractor Ltd wa Sh 2,006,532,500 kwa ujenzi wa barabara zilizopo katika manispaa hiyo.
“Katika utekelezaji wa mkataba huo kuliongezeka kazi zenye nyongeza za jumla ya Sh 1,077,189,040 ambapo jumla ya kiasi cha Sh 959,756,769 kilishalipiwa kwa kazi zilizoongezeka na b do mkandarasi alidai Sh 117,432,271.
“Kazi hizi ni za nyongeza zilizofanyika na kulipwa, hazikutolewa kwa kufuata kanuni, sheria na taratibu za manunuzi, idara ya ujenzi haikupata kibali cha bodi ya zabuni ya manispaa hiyo cha kuendelea na kazi hiyo ya nyongeza ,” alidai Mwakasege.
Alidai watuhumiwa wametumia mamlaka yao vibaya kinyume na kifungu cha 31 cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa Na 11/2007 na kwenda kinyume na kanuni namba 61(2) na 61(4) na tangazo la Serikali namba 446 la mwaka 2013 kwa kuruhusu kazi ya nyongeza kufanyika bila kupata kibali cha Bodi ya Zabuni ya Manispaa.
“Uchunguzi umekamilika na watuhumiwa watafikishwa mahakamani, watafunguliwa mashtaka kwa kosa la matumizi mabaya ya madaraka kinyume na kifungu cha 31 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na 11/2007 na kula njama kutenda kosa kinyume na kifungu cha 32 cha sheria ya kuzuia na kupambana na Rushwa Na 11/2007,” alieleza Mwakasege