Home | Terms & Conditions | Help

November 29, 2024, 1:32 pm

NEWS: MKURUGENZI JIJI LA TANGA AWATIMUA MADIWANI 4 WA CUF

Tanga: Mkurugenzi wa halimashauri ya Jiji la Tanga, jana jioni (09 Julai 2018) ametangaza kuwafukuza udiwani, madiwani wanne wa chama cha wananchi (CUF), ambao kati yao wawili wakiwa ni madiwani wa kuchaguliwa kwenye kata (akiwemo diwani ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Wilaya ya Tanga Mjini wa chama chetu), madiwani wawili ni wa Viti Maalum.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Leo July 10 na Mwenyekiti wa Baraza la Uwongozi wa chama cha CUF Julius Mtatiro amesema kuwa

Mkurugenzi amechukua uamuzi huo baada ya kupokea barua ya Naibu katibu mkuu wa chama hicho Magdalena Sakaya ya kuwavua uwanachama madiwani hao,

"CCM na Dola wanamtumia Sakaya ipasavyo (kupitia kwa Lipumba) ili kuhakikisha hadi mwaka 2020 maeneo ambayo CUF ina nguvu sana, madiwani na wabunge wawe wamesambaratishwa ili kuirahisishia kazi CCM,

Mtatiro amewataka wanachama wa chama hicho kuwa wavumilivu wakati Uwongozi wa CUF Unashughulikia jambo hilo kisheria

"Kwa sababu jambo hili limetokea ghafla, na likifanywa na vibaraka ambao CCM na Dola inalazimisha kuwakaimisha uongozi wa chama, mawakili wameanza hatua za kisheria ili kupambana dhidi ya jambo hilo"

Aidha Mtatiro ameongeza kuwa Taarifa walizonazo zinaonesha kwamba, tayari CCM na Dola vimeshaielekeza Tume ya Taifa ya Uchaguzi kutangaza kata hizo kuwa wazi ndani ya wiki ijayo ili uchaguzi ufanyike haraka na madiwani wapya wa CCM washinde. Pia, Lipumba ametakiwa kupeleka madiwani wa viti maalum wawili haraka sana na kuhakikisha kuwa madiwani hao wanakuwa wale wanaoiunga mkono CCM.