Home | Terms & Conditions | Help

November 30, 2024, 1:52 pm

NEWS: MKE WA TRUMP AFANYIWA UPASUAJI WA FIGO

Maryland: Mke wa Rais wa Marekani wa Sasa Donald Trump, Bi Melania Trump amefanyiwa upasuaji wa figo katika hospitali ya Walter Reed National Military Medical Center katika Mji wa Bethesda, Maryland.

Upasuji huo ulikuwa wenye mafaninikio na hakukuwa na matatizo yoyote kwa mujibu wa msemaji wake.

Bi Trump, 48, anatarajiwa kutumia muda mwingi wiki hii kupata nafuu hospitalini huko Maryland.

Rais Trump aliandika katika Twitter kuwa alikuwa njiani kwenda kumtembelea hospitalini.

Wiki iliyopita Bi Trump alizindua mpango kwa jina "Be Best" wenye lengo la kuwafunza watoto kuhusu masuala ya kijamii, afya kuhusu hisia na kimwili.

Alisema kampeni hiyo ina lengo la kuhakikisha maisha yenye afya na kuzuia dhuluma.

Pia ilitangazwa Jumatatu kuwa aliyekuwa kiongozi wa wengi wa seneti wa chama cha Democratic Harry Reid, 78, alikuwa amefanyiwa upasuaji wa kongosho.

Familia ya Bw Reid ilisema madaktari kwenye hospitali ya Johns Hopkins Hospital huko Baltimore walikuwa na uhakika kuwa upasuaji huo ulikuwa wenye mafanikio na anapata nafuu vizuri.

Madaktari walikuwa wamegundua tatizo mapema wakati wa uchunguzi wa kawaida wa kiafaya, kwa mujibu wa taaarifa.

Seneta wa Republican John MacCain ambaye mwenyewe anaugua saratani ya ubongo ni kati ya wale waliomtumia ujumbe wa heri njema.