- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MGAHAWA WA BUNGE WAKAMATWA NA SAMAKI HARAMU
Dodoma: Wizara ya Mifugo na Uvuvi imekamata samaki HARAMU kilo mbili kati ya 100 waliokuwa wakiuzwa kinyume cha sheria katika mgahawa wa ofisi ya Bunge jijini Dodoma.
Akizungumza leo Juni 19, Kaimu Meneja wa Uhifadhi wa Bahari na Maeneo Tengefu wa wizara hiyo, John Komakoma amesema samaki hao ni wale ambao kisheria hawapaswi kuvuliwa. “Mmiliki wa mgahawa huu amekiri kosa na kisheria tumemtoza Sh300,000 ambayo atakwenda kulipia benki,” amesema Komakoma.
Msemaji wa wizara hiyo, John Mpepele amesema aliyewapa taarifa za kuwepo samaki hao ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina aliyekuja kwenye mgahawa huo jana asubuhi.
“Alipowaona hawa samaki, akawatilia shaka na kutuagiza kuja kufuatilia,” amesema. Daniel Labiaramba alikiri kosa. “Nakiri kosa kweli lakini katika kilo 100 nilizonunua, ni ngumu kujua kama umewekewa samaki hawa, sikufanya hivi makusudi, kwani sikujua,”amesema