- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MATUMIZI YA MB NA M-PESA YAMEWAPA FAIDA VODACOM YA SH BIL 170
Dar es salaam: Matumizi ya data na M-pesa kwa watumiaji wa mtandao wa Vodacom Tanzania kwa mwaka 2017/2018 umeipatia mtandao huo mapato ya jumla ya Tsh. 432.2BIL yaliyo pelekea kuleta faida ya Tsh bilioni 170 kutoka Sh bilioni 47.554, mwaka 2016/17.
Akitangaza faida hiyo , Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom, Ian Ferrao amesema faida hiyo imetokana na faida ya uendeshaji wa M-Pesa na data.
Amesema mapato ya M-Pesa yameongezeka kwa asilimia 16.7, hadi kufikia Sh bilioni 291.193 kutoka Sh bilioni 246 mwaka jana ambapo jumla ya Dola za Marekani milioni 17.5 (Zaidi ya shilingi trilioni 39.5) zililipwa kupitia M-Pesa.
“Manunuzi ya data, yameongezeka kwa asilimia 34.7 ya Sh bilioni 141.61 kutoka bilioni 105.118 kwa mwaka uliotangulia, wateja wakiongezeka kutoka 882,000 hadi kufikia milioni 7.3, hii ikichagizwa na uwekezaji wa Sh bilioni 159. 7 ambao Vodacom imeufanya kwa ajili ya kutanua utoaji huduma wa Mtandao wa ‘4G’ kwa wateja wake katika mikoa mitano,” amesema.
Ferrao amesema mapato kutoka M-Pesa, Data na ujumbe mfupi pamoja na mapato ya uuzaji wa minara ya Vodacom kwa kampuni ya Helios Towers, yalitosha kuziba pengo lililotokana na kupungua kwa upigaji simu kutoka kwa wateja wa kampuni hiyo.
“Tunapoendelea mbele, tunaamini kwamba wateja wetu wa M-Pesa watazidi kuongezeka haswa kwa sababu tunazidi kutanua wigo wetu wa M-Pesa kwa kuongeza huduma ya Lipa kwa M-Pesa, hususani kwa kushirikiana na mabenki,” amesema Ferrao.