Home | Terms & Conditions | Help

November 23, 2024, 4:57 pm

News: Marekani yatofautiana na China kuhusu Makombora ya Korea ya Kaskazini

Washington: Maafisa wa Marekani wamepinga pendekezo ya serekali ya Beijini dhidi ya Korea Kaskazini kuwa huenda itasitisha majaribio yake ya makombora na yale ya Kinyuklia iwapo Marekani itasitisha vitendo vyake katika eneo hilo la Ukanda wa Asia

Ikitoa taarifa mapema leo Idara ya maswala ya kigeni nchini humo imesema kuwa mpango huo hautasaidia huku balozi wa Marekani kwa Umoja wa Mataifa Bi Nikki Halley amesema kuwa Korea Kaskazini haifikirii hatua hiyo anayo zungumzia china. Pendekezo hilo la China linajiri baada ya Korea kaskazini kufanya majaribio ya makombora yake manne ikiwa ni ukiukaji wa vikwazo vya kimataifa.

Wakati huohuo, Marekani imeanza kupeleka mfumo wa kujilinda dhidi ya makombora nchini Korea Kusini.

Pia inaendela na mazoezi ya pamoja na wanajeshi wa Korea Kusini hatua inayokasirisha Korea kaskazini.