Home | Terms & Conditions | Help

November 23, 2024, 11:04 pm

News: Maporomoko yasababisha zaidi ya watu 236 kupoteza maisha huko Colombia

Maporomoko ya matope yaliyo tokea kusini mwa Colombia imefikia 234. Taarifa hiyo imetolewa na shirika la msalaba mwekundu nchini humo ambalo limesema watu 202 wamejeruhiwa, zaidi ya 100 hawajulikani waliko, familia 300 zimeathirika na nyumba 25 zimeharibiwa.

Eneo lililoathirika vibaya zaidi na maporomoko hayo ya matope yaliyosababishwa na mvua kubwa iliyovunja kingo za mito mitatu ni mji wa Mocoa.Hapo jana, Rais Juan Manuel Santos alitangaza hali ya tahadhari eneo hilo na kusafiri kuangalia shughuli za uokozi. Vikosi vya wafanyakazi wanaoendesha shughuli za uokozi wanasema nyingi ya barabara hazipitiki. Zaidi ya maafisa 1,000 wakiwemo Wanajeshi na polisi wanasaidia katika shughuli za uokozi.

Jishi la colombia likifanya uwokoaji

Katika kipindi cha saa tatu , asilimia 30 ya mvua ambayo hunyesha mjini Mocoa, kwa mwezi ilinyesha kwa saa hizo tatu, kiasi ambacho kingenyesha kwa siku takriban 10, kwa hiyo ilikua mvua ya kumshtua kila mtu