- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS : MAPAMBANO SOMALIA YAMEUWA TAKRIBANI WATU 13
Mapambano huko kati kati ya Somalia yaliyotokea Jumamosi yalianza baada ya wanamgambo waliokuwa na silaha wa kundi la Al- Shabaab walipojaribu kuweka kodi kwa wakazi wa Halfoley, kijiji kimoja kilicho karibu na mji wa Jalalagsi katika wilaya ya Hiran.
Mkuu wa wilaya katika mji wa Bulabarde, Abdi Dahir Guure aliaambia Sauti ya Amerika-VOA kwamba wanajeshi wa serikali wanaowasaidia wafugaji walishiriki katika mapambano makali ya zaidi ya saa tano za ufyatuaji risasi na wanamgambo.
Maafisa wa serikali ya Somalia katika wilaya walisema vitengo vingine vya jeshi la taifa la Somalia viliingia katika vijiji vingine kwenye wilaya hiyo kuwazuia wanamgambo kujipanga tena na kufanya tena mashambulizi yanayosababisha vifo na uharibifu