- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MAMALISHE AKAMATWA NA KILO 7 ZA MADINI YA TANZANITE
Mamalishe mmoja mkazi wa mji mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro mkoani Manyara, alikamatwa akituhumiwa kukamatwa na kilo 7.53 za madini hayo yaliyofichwa chini ya unga uliokuwa kwenye ndoo.
Alikamatwa baada ya kupekuliwa na maofisa madini, maofisa usalama wa Taifa na polisi kwenye lango la kuingia ndani ya ukuta unaozunguka migodi ya madini ya Tanzanite.
Inadaiwa mamalishe huyo alipewa madini hayo na dalali kwa ajili ya kuyatorosha kupitia ndoo iliyokuwa na unga wa kupika ugali.
Akizungumzia tukio hilo jana, mkuu wa Wilaya ya Simanjiro, Zephania Chaula alisema mbali ya mamalishe huyo, mtu mwingine mmoja amekamatwa.
Chaula alisema mamalishe huyo anajishughulisha pia na kazi ya kuchekecha mchanga na udalali wa madini.
“Huyu dalali wa madini kwenye kitambulisho cha mpiga kura ameandika jina la Joshua Aguta na katika leseni ya udalali wa madini ameandika Midumbi Ojijo,” alisema Chaula.
Alisema baada ya kukamatwa na kuhojiwa mama lishe huyo alimtaja mhusika aliyempa madini hayo ambaye alipigiwa simu na kutakiwa kufika getini.
“Pale getini vijana wapo vizuri katika kutimiza wajibu wao kwa kuwa hata ukificha kwenye matunda watabaini tu,” alisema Chaula.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Agostino Senga alikiri kushikiliwa kwa watuhumiwa wawili kwa kudaiwa kutorosha madini hayo
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti juzi alisema hakuna utoroshaji wa madini hayo uliofanyika na kusababisha mrabaha kushuka kutoka Sh444 milioni hadi Sh40 milioni kwa mwezi, bali tatizo ni uzalishaji mdogo.
Mnyeti alisema hayo juzi alipozungumza na gazeti hili kuhusu taarifa ya tume ya madini iliyoundwa na Rais iliyosema utoroshwaji wa madini hayo umesababisha kushuka fedha za mrabaha.