Home | Terms & Conditions | Help

November 23, 2024, 3:14 pm

News: Majeshi ya ECOWAS yako mpakani mwa Gambia tayari kwa kumvamia Yahya Jammeh

Dar es salaam: siku chache baada ya Rais anaemaliza muda wake nchini Gambia kutangaza hali ya hatari baada ya kusikia kuwepo kwa majeshi ya ECOWAS, Leo hii majeshi hayo yako tayari kwa kuingia chini Gambia

Msemaji wa jeshi la Senegal amesema majeshi ya nchi hiyo yako katika mpaka na Gambia , na yataingia nchini humo , iwapo Rais Yahya Jammeh atakataa kuachia madaraka.

Ghana pia imesema itatuma zaidi ya wanajeshi 200 kumlazimisha Jammeh kuondoka madarakani. Nchi hizo ni sehemu ya mataifa ya Jumuiya ya uchumi ya Afrika magharibi ECOWAS ambayo yametishia kumuwekea Jammeh vikwazo ama kuingilia kijeshi nchini mwake iwapo hataondoka madarakani ifikapo usiku wa manane saa za eneo hilo.

Jammeh alishindwa uchaguzi wa Desemba mosi dhidi ya kiongozi wa upinzani Adama Barrow. Wakati huo huo Rais wa Mauritania Mohamed Ould Abdel Aziz amekwenda Senegal kukutana na Rais Macky Sall baada ya mazungumzo ya dakika za mwisho nchini Gambia yenye lengo la kuutatua mzozo wa kukabidhiana mdaraka.