- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MAJARIBIO YA CHANJO YA CORONA YAONYESHA MATUMAINI MAKUBWA
Habari njema duniani ni kwamba Chanjo ya virusi vya Corona inayofanyiwa uchunguzi na wanasayansi nguli kutoka chuo kikuu cha Oxford nchini Uingereza imeonyesha kwamba ina nguvu za kuongeza nguvu ya kinga mwilini, kulingana na majaribio ya utafiti wa hatua za awali yaliyofanywa hivi karibuni.
Matokeo yaliyochapishwa Jumatatu katika jarida la madawa la Uingereza, The Lancet, yalionyesha chanjo inayofanyiwa majaribio na kampuni ya madawa ya Astra-Zeneca na chuo kikuu cha OXFORD, ilitoa majibu mazuri kote kwenye seli zinazopambana na maradhi Pamoja na seli muhimu kwenye mfumo wa kinga zijulikanazo kama T-cells.
Majaribio hayo ni sehemu ya hatua ya pili ya uchunguzi wa chou cha Oxford, ambao haukuangalia iwapo chanjo inazuia dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona, swali ambalo litajibiwa kwenye hatua ya tatu ya majaribio ambayo tayari imeshaanza.
Tunahitaji utafiti zaidi ili kubaini iwapo chanjo hii inatoa kinga kamili kwa mtu aliyeambukizwa virusi vya Corona, na iwapo inatoa kinga, ni kwa muda gani, alisema Andrew Pollard, ambaye alitayarisha roipoti kuhusu utafiti wa chuo cha Oxford.