- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MAITI YAZINDUKA IKIWA MONCHWARI
Nchini Africa kusini Mwanamke mmoja ameacha watu midomo wazi baada ya kupatikana akiwa hai katika jokofu la kuhifadhia maiti.
Mwanamke huyo alifikishwa katika chumba hicho baada ya madaktari kusema alikuwa amefariki dunia kufuatia ajali ya barabarani.
Katika uchunguzi wao madaktari walisema hakuonyesha dalili zozote za kuwa hai na hivyo kutamka kuwa alikuwa amepoteza maisha.
Mafundi wanaofanya kazi katika chumba hicho ndio waliogundua kuwa mwanamke huyo alikuwa hai na hatimaye kumwondoa.
Aliletwa kwenye chumba hicho akidhaniwa amepoteza maisha yeye na wenzake wawili baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupinduka na kuvingirika zaidi ya mara tatu. Wawili hao waliobakia ndiyo waliofariki dunia.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la AFP, mwanamke huyo ambaye hakutajwa jina lake sasa amekuwa akipokea matibabu katika Hospitali ya Leratong iliyoko Magharibi mwa mji wa Johannesburg.
Familia ya mwanamke huyo aliyegunduliwa kuwa hai imesema wamepata mshtuko na wana wasiwasi mkubwa kuhusu mkasa huo