Home | Terms & Conditions | Help

November 23, 2024, 7:44 pm

News: Maiti ya zikwa kwenye ofisi ya Diwani Shinyanga

Kahama; Mtoto wa kata ya mhongolo mjini kahama aliyefariki dunia alisababisha wananchi wa kata hiyo kuandamana bila kibali wakiwa na jeneza la mtoto huyo kwa lego la kwenda kuuzika mwili huo kwenye ofisi ya kata hiyo wakidai diwani wa kata Michael Mizubo ameuza eneo la makaburi kwa maslahi yake binafsi.

Akizingumza na muakilishi media mwananchi mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja la Paulina ambaye ni miongoni mwa watu waliokuwa kwenye maandamano hayo alisema waliamuwa kwenda kuuzika mwili huo wa mtoto huyo alijulikana kwa jina la Rosemary aliyefariki kwa ugonjwa wa kawaida kwenye ofisi hiyo ya kata kwa sababu hakuna eneo la kuzikia .

Lakini vilevile wakati wanachimba kaburi hilo kwenye mlango wa ofisi ya diwani huyo kwa lengo lakuuzika mwili huo polisi walifika na kuwatawanya kwenye eneo hilo kwa madai ni ukiukaji wa taratibu .

Naye diwani wa kata hiyo Mizubo anayedaiwa kuuza eneo la maziko amesema wananchi hao walikuwa nasababu zao za kisiasa kwani pamoja na eneo hilo la makaburi kuuzwa tayari kuna eneo jingine limetengwa kwa ajili ya maziko.