- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MAHAKAMA YATUPILIA MBALI OMBI LA VIONGOZI WA CHADEMA
Dar es salaam: MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Jana June 12 imetupilia mbali ombi la upande wa utetezi katika kesi ya uchochezi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema na wenzake saba lililokuwa linatoa taarifa ya kusudio la kukata rufaa dhidi ya uamuzi mdogo uliotolewa mahakamani hapo jana.
Hatua hiyo imekuja baada ya upande wa mashtaka Juni 11 mwaka 2018 kuamuriwa na Mahakama wafanye marekebisho katika hati ya mashtaka baada dhidi ya washtakiwa hao badaa ya hati hiyo, kuonekana kuwa na mashtaka batili na yenye mapungufu ya kisheria.
Kutokana na kutupwa kwa kusudio hilo la kukata rufaa, washtakiwa hao wamesomewa mashtaka mapya 13 na na Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri.
Mbali na Mbowe, washtakiwa wengine ni, mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Salum Mwalimu na Naibu katibu Mkuu Bara na Mbunge wa Kibamba John Mnyika.
Katibu wa chama hicho Dk.Vicenti Mashinji, Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Mbunge wa Kawe Halima Mdee na mbunge wa bunda, Esther Bulaya.
Katika mashtaka hayo mapya yaliyofanyiwa marekebisho, imedaiwa washtakiwa hao, kwa pamoja Februari 1 na 16 mwaka 2018, Dar es Salaam washtakiwa pamoja na wenzao ambao hawapo mahakamani walikula njama ya kutenda kosa la kufanya mkusanyiko usio halali, mkusanyiko wenye ghasia na kukiuka tamko kutawanyika.
Pia imedaiwa, siku hiyo katika viwanja vya buibui na Mwananyamala Wilaya ya Kinondoni washtakiwa hao wakiwa wamekusanyika na adhma ya pamoja, waliitekeleza adhma yao kwa kufanya mkusanyiko usio halali na kusababisha watu waogope kuwa watakwenda kupelekea uvunjïfu wa amani.
Pia watuhumiwa hao wanadaiwa kutekeleza mkusanyiko ama maandamano yasiyo halali wakiwa na lengo la kuvamia ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni na kuleta hofu ya uvunjifu wa amani.