Home | Terms & Conditions | Help

November 23, 2024, 6:59 pm

NEWS: MAHAKAMA YAAMURU TANZANIA KURUHUSU KUPINGWA MATOKEO YA URAIS

Hatimaye Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu imeiamuru Tanzania kuviruhusu vyama vya siasa nchini humo kupinga matokeo ya uchaguzi wa rais Mahakamani baada ya kutangazwa na tume ya taifa ya UCHAGUZI ya nchi hiyo.

NEC yatangaza majimbo matatu ya uchaguzi

kwa mujibu wa sheria ya Tanzania hairuhusu mahakama kuhoji wala kupinga matokeo ya urais mara mshindi wa uchaguzi atakapokuwa ametangazwa na tume ya uchaguzi

Hukumu hiyo ilitolewa jana na Mahakama hiyo, yenye makao yake makuu jijini Arusha, Kaskazini mwa Tanzania, imeitaka Tanzania kuchukua hatua "za muhimu za kikatiba na za kisheria, ndani ya muda mwafaka" kubadilisha sheria hiyo inayozuia kupingwa kwa matokeo ya urais

Kesi hii ilipelekwa mahakamani hapo na mwanasheria MATATA wa haki za binadamu nchini humo Bw.Jebra Kambole ambaye alihoji kwamba kifungu hicho cha sheria kinachozuia kupingwa kwa matokeo ya uchaguzi wa urais kinakiuka haki zake za msingi

Uamuzi huu wa mahakama ya Afrika unakuja wakati ambao matokeo ya uchaguzi wa urais ya nchi za jirani za Kenya na Malawi yalipingwa mahakamani na mahakama kuamuru marudio ya chaguzi hizo

Wakati marudio ya uchaguzi wa nchini Kenya yalisusiwa na vyama vya upinzani nchini humo, kurudiwa kwa uchaguzi nchini Malawi kulipelekea muungano wa vyama vya upinzani kushinda

Hata hivyo kutokana na siku chache kubakia hadi uchaguzi mkuu kufanyika, kuna uwezekano mdogo wa mabadiliko hayo kufanyika juu ya uchaguzi wa mwaka huu.