Home | Terms & Conditions | Help

November 30, 2024, 1:37 pm

NEWS: MAHAKAMA YA KENYA YAKATAA WANANDOA KUGAWANA MALI SAWA

Jaji wa mahakama kuu John Mativo amepinga wanandoa kugawana mali nusu kwa nusu wanapo achana kwa talaka.

Jaji Mativo amesema, wanandoa wanapoachana wana haki ya kuchukua kile walichochangia tu kifedha katika ndoa hiyo

Umauzi huo unaambatana na sheria ya ndoa nchini ambayo shirikisho la mawakili wanawake Kenya FIDA lmekuwa likifanya kampeni ifutiliwe mbali.

Kumekuwa na mjadala mkubwa nchini ikiwemo pia katika mitandao ya kijamii wakati uamuzi huo umepitishwa huku kukiwa na visa vingi vya watu mashuhuri kutalikiana.

Kundi hilo linalotetea haki za usawa wa kijinsia limelalamika kuwa sheria hiyo inawanyanyasa wanawake, likidai kuwa kwa mara nyingi wanawake ndio hubeba mzigo mzito wa kulea watoto wakati talaka zinapopita.

Lakini jaji huyo leo itakuwa sio haki mtu kupata zaidi ya walichochangia wakati ndoa inapovunjika.

Kesi hiyo imefuatiliwa kwa makini na Wakenya wengi walioelezea hisia zao kupitia mitandao ya kijamii.

Mahakama imesema iwapo itaruhusu ombi hilo la FIDA, itatoa mwanya kuruhusu wanaoatafuta kujitajirisha kuingia katika ndoa kwa lengo la kujinufaisha.

Jaji amesema sheria haiwanyanyasi wanawake kwasababu umauzi huu pia utakuwa na manufaa na kuwalinda wale wanaofanya kazi kwa bidii na kuunda mali ya familia.