- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
News: Magufuli amemtumbua Kigogo mwingine Serekalini
Dodoma: RAIS John Magufuli ametengua uteuzi na kumsimamisha kazi Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Bunge, Uledi Mussa.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, John Kijazi, kutoka Ikulu ya Chamwino, Dodoma, ilieleza kuwa kutenguliwa kwa uteuzi na kusimamishwa kazi kwa Uledi, kulianza jana.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, hatua hiyo imechukuliwa ili kupisha uchunguzi zaidi dhidi ya Uledi Mussa, kwa kutozingatiwa taratibu zinazotakiwa katika kushughulikia masuala ya uwekezaji.
Siku chache zilizopita Rais Magufuli alikutana na kuzungumza kwa faragha na wabunge wote wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Alikutana nao mwishoni mwa wiki, ambapo waandishi wa habari hawakuruhusiwa na pia wabunge wote hawakuruhusiwa kuingia na simu.
Kadhalika, Rais Magufuli alikutana na Baraza lake la Mawaziri jana. Uledi Mussa ni mmoja wa makatibu wakuu 29, walioteuliwa na Rais Desemba 30, 2015, baada ya kumalizika kwa Ucha guzi Mkuu#habarileo