- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MAGARI YAZUILIWA KUINGIA MERERANI KUEPUSHA KUTOROSHA MADINI
Mirerani. kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Manyara imezuia magari kuingia ndani ya ukuta wa mererani unaozunguka migodi ya madini hayo.
Hii ni Baada ya Tume ya Madini iliyoundwa na Rais John Magufuli kubaini utoroshwaji wa madini ya Tanzanite katika mji mdogo wa Mirerani,
Jana alinukuliwa mwenyekiti wa tume hiyo, Profesa Idris Kikula akisema kuwa utoroshaji wa madini hayo ya vito umesababisha mrabaha kushuka kutoka Sh444 milioni hadi Sh40 milioni kwa mwezi.
Hadi kufikia saa 7:00 mchana jana, magari yaliyokuwa yamebeba maji pamoja na yaliyobeba wachimbaji na wanunuzi yali zuiwa kuingia migodini.
Pia, wachimbaji wadogo walizuiwa kutumia lango hilo kuingia migodini, wakitakiwa kuonyesha vitambulisha vya Taifa na vile vinavyotolewa na Wizara ya Madini, hali iliyoibua mtafaruku kutokana na wengi kutokuwa navyo.