- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
News: Machinga wafunga mitaa ya Dar es salaam Baada ya kauli ya Rais John Magufuli kuwaruhusu
Dar es saam: hiyo imetokea siku moja baada ya Rais Dk. John Magufuli kutoa agizo kwa wakuu wa mikoa na wilaya kutowafukuza maeneo ya katikati ya miji wafanyabiashara maarufu kama machingi.
Mapema asubuhi jana Dar es Salaam, MUAKILISHI lilishuhudia mitaa kadhaa ya Kariakoo tayari wafanyabiashara hao wameweka shehena kubwa za bidhaa, huku wakiendelea kuzitandaza pembezoni na hata katikati ya barabara bila kujali wapitanjia wengine, hususani wanaotumia vyombo vya moto.
Mitaa iliyosheheni wafanyabiashara hao ni Kongo, Nyamwezi, Swahili, Sikukuu, Narung’ombe na Mchikichi.
Baadhi ya wafanyabiashara wa maduka walionekana kuduwaa, huku wengine nao wakihaha kutafuta nafasi za kutandaza bidhaa zao nje.
Wamachinga wengine walipanga bidhaa zao katikati ya barabara na kuacha sehemu ya kupita tairi za gari. Hali iliyofanya bidhaa zao kuwa uvunguni mwa gari.
Mmoja wa wamachinga walioweka bidhaa katikati ya barabara, Mtaa wa Kongo, aliyejitambulisha kwa jina moja la Robert, aliliambia MTANZANIA kuwa mtaa huo ndio wenye wateja wengi, hivyo wanalazimika kugombania nafasi za kupanga biashara zao.
Msemaji wa wamachinga wa Kariakoo, Masoud Issa, alisema wanamshukuru Rais Magufuli kwa kuwaruhusu kufanya biashara zao katikati ya miji.
“Tunamshukuru na kumpongeza Rais Magufuli kwani amekuwa mtu wa mfano kwa kuwakumbuka wamachinga, ambao kwa miaka mingi tumekuwa tukionekana watu wasio na thamani wala akili,” alisema Issa.
Hata hivyo, Issa alisema ruhusa hiyo ya rais inahitajika udhibiti kwa kuwa wapo wafanyabiashara wenye maduka, ambao wanatumia agizo la rais vibaya kwa kutoa bidhaa zao madukani na kuzitandaza barabarani ili wasilipe kodi.
“Kuna watu wanatafuta vijana wanatoa nje bidhaa zao madukani wanazimwaga barabarani, ambako wanajua hawatadaiwa risiri na hawatalipa kodi,” alisema Issa.
MAKONDA LAWAMANI
Kiongozi huyo wa wamachinga alimtupia lawama Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, kuwa alikuwa akirudisha nyuma juhudi za viongozi wa jiji hilo kupata mwafaka wa wamachinga.
Alisema tangu awali mapendekezo yao waliomba watengewe mitaa minne ya Kongo, Nyamwezi, Swahili na Sikukuu, huku wakiweka meza kwa mpangilio pembezoni mwa barabara na kuacha nafasi za watu kuingia madukani na kuweka mapipa ya taka.
“Katika mpango huo, pia tulisema tupo tayari tupewe mashine za kukusanya ushuru na kukagua risiti za wafanyabiashara ili Serikali ipate mapato yake, lakini RC Makonda alipinga mapendekezo hayo na kuyavuruga,” alisema.
SOKO LA ILALA
Katibu wa Ulinzi na Usalama Soko la Ilala, Yahya Makuani, alisema Rais Magufuli yuko sahihi, lakini kitu cha kuzingatia katika barabara za pembeni za waenda kwa miguu zisiguswe kwa sababu usumbufu utakuwa mkubwa.
“Kuna mitaa kama Kongo, Muhonda, Sikukuu na Mkunguni wapewe wamachinga, ifungwe wafanye biashara.
“Lakini wakiruhusiwa kufanya biashara pia wawajibike kulipa tozo ndogo ndogo kama tunavyolipa sokoni, sisi wanalipa Sh 500 kwa siku kila mfanyabiashara, hiyo inasaidia usafi na kuimarisha ulinzi, inaenda halmashauri,”alisema Yahya.
SIMU 2000
Wafanyabiashara wengi waliohamishiwa katika soko lililopo Kituo cha Mabasi Sinza (Simu 2000), wamerejea barabarani baada ya agizo hilo la Rais Magufuli juzi.
Awali walikuwa wakifanya biashara eneo la Ubungo kabla ya kuhamishiwa hapo na aliyekuwa Meya wa Kinondoni, Boniface Jacob.
Wafanyabiashara hao waliondoka mapema jana na kurudi barabarani kuanzia njiapanda ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam hadi Ubungo Mataa.
Akizungumza na MTANZANIA, Meneja wa soko hilo, Elichilia Hamis, alisema wafanyabiashara hao walianza kuondoka mapema asubuhi jana kurudi katika maeneo ya barabarani.
“Wengi wameondoka na kurudi barabarani, ambako awali waliondolewa na meya, vizimba vingi vimebaki wazi, katika baraza F, B na D ni kweupe kabisa, baraza E na C wamepungua mno na wale wakina mama waliokuwa wakiuza chakula wote wameondoka kabisa,” alisema.
Alisema katika soko hilo walikuwa na uwezo wa kukusanya mapato hadi Sh milioni nane kwa mwezi, lakini kwa hali ilivyo sasa mapato yanaweza kupungua,” alisema Hamis.
Kwa msaada wa MTANZANIA