- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
News: Maandamano ya kumpinga Trump baada ya kupiga marufuku kuingia kwa waislam yaongezeka zaidi
Washington: Mamia kwa maelfu ya watu waendelea kuandamana katika miji nchini Marekani na katika viwanja vya ndege jana kuelezea kuchukizwa kwao kuhusiana na amri za kiutendaji zinazochukuliwa na rais Donald Trump kuzuwia kuingia nchini humo kwa wasafiri wanaotoka katika mataifa saba yenye waislamu wengi. Mjini New York, Washington na Boston,
Wimbi la pili la waandamanaji lilifuatia maandamano ya papo kwa papo yaliyozuka katika viwanja vya ndege nchini Marekani siku ya Jumamosi wakati wafanyakazi wa ulinzi wa mipakani walipoanza kutekeleza amri ya Trump.
Maandamano hayo yalisambaa katika majimbo ya magharibi kwa siku nzima jana. Seneta kutoka chama cha Democratic Charles Schumer kutoka mjini New York aliliambia kundi la waandamanaji kwamba amri ya Trump ni kinyume na maadili ya Marekani na inakwenda kinyume na maadili ya msingi ya nchi hiyo.