Home | Terms & Conditions | Help

November 23, 2024, 3:58 pm

News: Maamuzi ya mahakama ya KISUTU kufuta kesi ya umeya Kinondoni

Dar es salaam: Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeifuta kesi ya matokeo ya umeya wa Manispaa ya Kinondoni,



Mahakama imefuta kesi hiyo leo baada ya kukubaliana na pingamizi la awali lililowekwa na meya wa manispaa hiyo, Benjamini Sitta kupitia kwa wakili wake, Baraka Nyambita.
Kesi hiyo namba 3 ya mwaka 2016 ilifunguliwa na aliyekuwa mgombea umeya katika manispaa hiyo kupitia Chadema, Mustafa Muro na aliyekuwa mgombea wa nafasi ya unaibu meya kupitia chama hucho, Jumanne Mbunju.