Lissu ambaye alikuwa Mbunge wa Singida Mashariki amesema kuwa pia anataka kuhudhuria Mkutano Mkuu utakaofanyika Julai 29, kwasababu mkutano huo ndio utakaompitisha mgombea Urais wa chama hicho kwenye Uchaguzi Mkuu, Oktoba 2020.
Tundu Lissu ni mmoja wa watia nia waliojitokeza kuwania nafasi ya Urais kupitia chama hicho kwenye Uchaguzi Mkuu, wengine ni wakiwemo, Mwenykiti wa chama, Freeman Mbowe, Mbunge Peter Msigwa na mwanasiasa Lazaro Nyalandu.
Lissu yupo Ughaibuni mara baada ya kunusurika kwa Jaribio la kuuwawa na watu wasio julikana Septemba 2017 Jijini Dodoma.
Rais huyo wa Zamani wa TLS hakuwahi kurudi nchini tena na hiyo itakuwa ni mara ya kwanza baada ya tukio la kushambuliwa kwake.