- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: LEMA AMWAMBIA SIRRO KUWA WABUNGE WA CCM NI VIGEUGEU
Mbunge wa Arusha mjini (CHADEMA) amemtahadharisha Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania (IGP) Simon Sirro kuwa anapaswa kufanya kazi yake kwa umakini sana kwani ipo siku wabunge wa CCM watamgeuka.
"IGP umeona mijadala bungeni, CCM hawana aibu nimekuwa nao bungeni kwa miaka nane, walipomsifu Seth wa IPTL na wengine nilikuwepo na walipokuja geuka nilishuhudia, tumeeleza uhalifu mkubwa dhidi ya ubinadamu, kuna siku uhalifu huu utakuwa hadharani. Play smart brother" alisema Godbless Lema
Lema ameyasema hayo Leo Mai 7 kupitia Ukurasa wake wa Twitter siku chache baada ya kuibuka kwa mijadala bungeni kuhusu mambo mbalimbali yanayoendelea nchini ikiwa pamoja na masuala ya ulinzi na usalama ambapo baadhi ya wabunge walilinyooshea vidole jeshi la polisi kushindwa kushughulikia baadhi ya mambo ikiwa pamoja na kuchunguza sakata la Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu kupigwa risasi, kutekwa na kupotea kwa baadhi ya watu akiwepo mwandishi wa habari Azory Gwanda, Ben Saanane na Simon Kanguye.