- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: KIONGOZI WA WAASI SUDAN KUREJEA KWENYE UMAKAMO WA RAIS
Hatimaye Kiongozi wa waasi nchini Sudani kusini Rieck Machar ameridhia kurudi kwenye wadhifa wake wa awali wa makamo wa raisi nchini Sudan Kusini baada ya makubaliano ya mgawanyo wa madaraka kufikiwa kati yake na raisi wa taifa hilo Salva Kiir.
Waziri wa mambo ya nje wa Sudan Al-Dierdiry Ahmed amethibitisha kuwa pande zote zimekubali kuwa na makamo wanne wa raisi,wawili waliopo sasa lakini pia Rieck Machar kurejea katika nafsi hiyo na nafasi ya nne itajazwa na mwanamke atakayechaguliwa kutoka upande wa upinzani.
Hatua hiyo imefikiwa katika majadiliano ya siri yaliyofanyika mjini Kampala nchini Uganda.
Makubaliano ya sasa ni sehemu ya jitihada za jumuiya ya kikanda kufufua mazungumzo ya amani yaliyolenga kumaliza mzozo uliogharimu maisha ya maelfu ya raia na mamilioni kukimbia makazi yao tangu Decemba 2013.
Vita ilianza baada ya raisi Kiir kumtuhumu aliyekuwa makamo wake Machar,kuwa aliandaa njama za kumpindua.