Home | Terms & Conditions | Help

November 29, 2024, 7:41 pm

NEWS: KESI YA VIONGOZI WA CHADEMA YAKWAMA MAHAKAMANI

Dar es salaam: Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeshindwa kuendelea na kesi inayowakabili viongozi wa chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA kwa sababu ya Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe kufiwa na kaka yake.

Washtakiwa walitarajiwa kusomewa maelezo ya awali (Ph) mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri, ambapo Wakili wa serikali Mkuu, Faraja Nchimbi amedai kuwa kesi hiyo imeitishwa kwa ajili ya Ph, lakini mshtakiwa wa kwanza Mbowe na Matiko hawapo mahakamani.

Mahakama hiyo imeagiza mshtakiwa wa 5, Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko kuhakikisha anafika mahakamani katika tarehe ijayo kinyume na hapo atachukuliwa hatua.

Mbali na Mbowe, mwingine ni Mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Salum Mwalimu na Naibu katibu Mkuu bara na Mbunge wa kibamba John Mnyika, Katibu wa chama hicho Dk.Vicenti Mashinji, Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Mbunge wa Kawe Halima Mdee na mbunge wa bunda, Esther Bulaya.

Kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 13 ikiwemo kula njama, ambapo inadaiwa February 1 na 16, 2018, Dar es Salaam walikuĺa njama ya kutenda kosa la kufanya mkusanyiko usio halali na kukiuka tamko kutawanyika.

Wanadaiwa kuwa February 16,2018 katika barabara ya Kawawa Kinondoni Mkwajuni washtakiwa hao wakiwa na wenzao 12 ambao hawapo mahakamani walikiuka tamko la kuwataka kutawanyika la Afisa wa polisi SSP, Gerald Ngiichi kwa kugoma kutawanyika na kupelekea uvunjifu wa amani.