- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: KESI YA MMILIKI WA TP MAZEMBE MOISE KATUMBI YAANZA KUSIKILIZWA
DRC: Kesi inayohusu askari mamluki ambapo anahusishwa na Moise Katumbi Chapwe, ambae ni gavana wa zamani wa Katanga imeanza kusikilizwa jana Jumatano june 27 mbele ya Mahakama Kuu mjini Kinshasa, mji mkuu wa DRC.
Mamia ya wafuasi na wapenzi wa mwanasiasa huyo wa upinzani wamehudhuria kesi hiyo.
Gavana wa zamani wa Katanga anashutumiwa "kuhatarisha usalama wa taifa DRC".
"Katumbi ambaye alitangaza kuwania katika kinyang'anyiro cha urais manmo Desemba 23, 2018 anashutumiwa kuajiri askari mamluki kwa lengo la kuhatarisha usalama wa nchi.
Moise Katumbi ambaye yuko uhamishoni anashtumiwa katika kesi hiyo pamoja na watu wengine watano, ikiwa ni pamoja na raia mmoja kutoka Marekani.