Home | Terms & Conditions | Help

November 23, 2024, 6:50 pm

News: Kesi ya Masamaki Bado kisungumkuti

Dar es salaam: Kesi inayomkabili aliyekuwa Kamishna wa Forodha na Ushuru wa TRA, Tiagi Masamaki na wenzake, wanao shtakiwa kwa kosa la Kula njama kwa kuidanganya serekali ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania na kuisababishia serekali hasara ya shilingi 12.69 Bilioni.


Upande wa mashtaka katika kesi ya uhujumu uchumi kwa kula njama na kuisababishia serikali hasara utatoa taarifa za hatua za upelelezi ulipofikia Februari 3,2017.

Hayo yameelezwa Jana na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Vitalis Peter mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, wa Mahakama ya Mkazi Kisutu, Huruma Shaidi wakati kesi hiyo ilipotajwa mahakamani hapo.


Mbali na Masamaki washtakiwa wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo iliyotokana na sakata la makontena 329 ni Meneja Kitengo cha Huduma za Ushuru TRA, Habib Mponezya (45) na Meneja Msimamizi na Ufuatiliaji wa Forodha, Burton Mponezya (51).
Msimamizi Mkuu Kitengo cha Ushuru wa Forodha ICD Azam, Eliachi Mrema (31), Mchambuzi Mwandamizi wa Masuala ya Biashara TRA, Hamis Omary (48), Meneja wa Oparesheni za Usalama na Ulinzi ICD, Raymond Adolf Louis (39) na Meneja wa Azam ICD, Ashrafu Khan (59) na Haroun Mpande (28) wa kitengo cha Mawasiliano ya Kompyuta ICT TRA.

Kwa pamoja wanadaiwa kuwa kati ya Juni Mosi na Novemba 17, 2015 walikula njama kwa kuidanganya serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu Sh 12.7 bilioni.
Washtakiwa hao, wanadaiwa ku danganya kuwa Makontena 329 yaliyokuwepo katika Bandari Kavu ya Azam (AICD) yalitolewa baada ya kodi zote kufanyika wakati wakijua si kweli.