- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: KESI VIONGOZI WA CHADEMA BADO HAKIJAELEWEKA
Dar es salaam: Kesi Na. 112/2018 inayowakabili Viongozi Wakuu wa Chama na Wabunge 7 wa CHADEMA, imeaihirishwa hadi Julai 25 mwaka huu ili kusubiri maamuzi ya shauri Na. 126/2018 ya Washtakiwa yaliyopo Mahakama Kuu kanda ya Dar es salaam ya kuomba irejee kesi hiyo iliyopo Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu.
Julai 2 mwaka huu, Mbowe na wenzake wanane, walipeleka maombi wakitaka kubadilishiwa Hakimu anayesimamia kesi hiyo kwa madai kuwa, hawana imani naye.
Mbowe na wenzake, wanakabiliwa na mashtaka 12 ikiwamo kuchochea ghasia, kukaidi amri ya polisi, uchochezi na uasi.
Wanadaiwa kufanya makosa hayo, Februari 16 wakati polisi wakiwatawanya wafuasi wa Chadema waliokuwa wakiandamana. Katika tukio hilo, mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Chuo cha Usafirishaji (NIT) Akwilina Akwiline alipigwa risasi akiwa kwenye daladala, eneo la Kinondoni, Mkwajuni.
Wengine katika kesi hiyo ni Katibu Mkuu, Vincent Mashinji, Naibu Katibu Mkuu, bara, John Mnyika, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu, Mbunge wa Bunda, Esther Bulaya, Mbunge wa Tarime Mjini , Esther Matiko na mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa, Tarime Vijijini, John Heche na wa Kawe
Imeandikwa na Deyssa H. Issa
Na kuhaririwa na Merry Mgawe
Muakilishi Publisher