- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS : KENYA YAZIONYA NCHI ZA KIARABU ZIACHE KUSHADIDISHA MGOGORO WA SOMALIA
Serikali ya Kenya imezionya nchi za Kiarabu za Ghuba ya Uajemi, hasa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kuacha kuchochea mgogoro wa Somalia na kuidhoofisha serikali ya nchi hiyo.
Wiki hiliyopita, Kenya ilitangaza uungaji mkono wake kwa serikali ya Rais Mohamed Abdullahi 'Farmajo' wa Somalia na kuzikosoa kwa njia isiyo ya moja kwa moja nchi ambazo zina mikataba ya kibiashara na kijeshi na maeneo ya Somaliland na Puntland. Serikali ya Kenya inasema mikataba kama hiyo inaweza kuidhoofisha serikali ya Somalia.
Televisheni ya al Jazeera imewanukulu maafisa wa serikali ya Kenya waliohojiwa na gazeti la Sunday Nation wakisema, Kenya inataka jamii ya kimatiafa ishirkiane moja kwa moja na serikali ya Mogadishu sambamba na kuunga mkono jitihada za kuimarishwa uwezo wa vikosi vya usalama nchini humo.
Wiki iliyopita katika hotuba yake ya kila mwaka bungeni, Rais Uhuru Kenyatta aliashiria kwa njia ya moja kwa moja kuwa baadhi ya madola ya kigeni yanavuruga msingi wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika Somalia Amisom. Alisema lengo la uingiliaji huo ni kuidhoofisha serikali kuu ya Somalia.
Serikali ya Somalia imekataa kujiunga na Saudi Arabia, UAE, Bahrain na Misri katika kuitenga Qatar kwenye mgogoro unaotokota wa Ghuba ya Uajemi. Hatua hiyo ya serikali ya Mogadishu inaonekana kuzikasirisha tawala hizo ambazo sasa zinalenga kuidhoofisha serikali hiyo.
Serikali ya Somalia imewasilisha malalamiko ya kimatiafa dhidi ya UAE baada ya nchi hiyo kutia saini mkataba wa kijeshi na kibiashara na eneo lilolojitangazia uhuru la Somaliland.