- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: KATIBU : ''MIGOGORO HAILETI AFYA''
BAHI DOM: Uongozi wa halmashauri ya wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma umetakiwa kutambua , kuorodhesha na kutatua migogoro iliyopo katika halmashauri hiyo ilikuleta uhusiano mzuri na wananchi wake.
Akizungumza leo katika kikao maalum cha baraza la madiwani cha kujadili majibu ya menejimeti kuhusu hoja zilizotolewa namthibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali kwa mwaka wa fedha ulioishia tarehe 30 juni 2017 Kaimu Mkuu wa Mkoa ambaye pia ni Katibu Tawala mzaidizi wa Serikali za Mitaa Mkoani hapo Emmanuel Kuboja amesema migogoro ambayo mkuu huyo ameangizaifuatiliwe ni migogoro kati ya Mkurungezji na watendaji wake, madiwani kwa madiwani, watumishi kwa watumishi na yaardhi na kudai kuwa siku zote migogoro haijengihurudisha maendeleo nyuma.
Aidha amezitaka kamati za kudumu kusimamia na kutekeleza majukumu yake isavyo ili kuepuka maswali na Kuleta mrejesho mzuri katika vikao vyao.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo Danford Chisomi amesema wao wasiwe chanzo cha kuwagombanisha wananchi bali watafute njia ya kuweza kutatua tatizo hilo ikiwemo kukaa kuzungumza kama madiwani kabla ya kuwafikia na kuongeza kuwa kushindwa kutekelezeka kwa baadhi ya hoja ni kutoka na ushirikiano duni.
Naye Mkuu wa Wilaya hiyo Elizabeth Kitundu ameishauri kamati kipindi kijacho hoja zipunguzwe kwa kufuata taaratibu na sheria za halmashauri ili kupunguza mlolongo wa hoja hizo.
Awali akiwasilisha taarifa hiyo Mweka Hazina wa wilaya Saad Ishabailu amesemakatika mwaka 2014/2015 uwepo wa migogoro ya mipaka kati ya halmashauri na taasisi zingine za kiserikali kama halmashauri ya manispaa ya Dodoma, migogoro ya kati ya Nholi, Kingwena Mbabala hadi sasa halmasahauri imeshafuatilihoja hiyo ambapo wataalamu wa idara ya ardhi walifika katika maeneo husika na kubaini mipaka eneo lililokuwa linagombaniwa.
Hata hivyo Mkaguzimkuu wa Njeya Mkoa Chambi Sasamka ameipongeza wilayakwa kupata hati safina kuwatakakutoa ushirikiano kwa wakaguzi, ili kuendelea kuvuta kambana kupata tena hati safi.
Halmashauri ya wialaya ya Bahi ni miongoni mwa halmashauri nane zinazounda Mkoa wa Dodoma.