- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
News: Kaimu mkuu wa kitengo cha mawasiliano serikalini wa wizara taarifa kutoka vyombo vya dola Roma Mkatoliki hajashikiliwa na kituo chochote cha polisi
Dar es salam: Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, sanaa na Michezo imesema imepokea kwa mshtuko taarifa za kutoweka kwa Mwanamuziki Ibrahim Mussa kwa jina la kisanii “Roma Mkatoliki” tangu tarehe 5 Aprili 2017.
Katika taarifa yake iliyotolewa jana jioni na kusainiwa na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa wizara Zawadi Msalla, alisema kuwa wizara hiyo kwa dhamana yake katika tasnia ya sanaa, imefuatilia kwa karibu suala hilo kwa kuwa lina muelekeo wa jinai na kwamba hashikiliwi katika kituo chochote cha polisi.
"Hata hivyo taarifa kutoka vyombo vya dola zinathibitisha kuwa Roma Mkatoliki hashikiliwi katika kituo chochote cha polisi".Alisema Zawadi.
Alisema kutokana na hali hiyo, wizara imewaomba wadau mbalimbali na wananchi kwa ujumla kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa zozote zitakazo saidia kujua alipo msanii huyo.