- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
News: Jopo la viongozi wakubwa wajipanga kumdhibiti Magufuli
Dar es salaam: VITENDO vya Rais John Magufuli kutoa matamko yaliyo kinyume cha mila na desturi za kisiasa hapa nchini, kimeibua hofu kwa viongozi wastaafu nchini ambao sasa wanataka maadhimisho ya kitaifa yatungiwe sheria mahususi.
Tangu aingie madarakani mwaka 2015, Rais Magufuli ametoa matamko ya kubadilisha utaratibu wa kawaida wa kuadhimisha sherehe za kitaifa, kuhusu uwezekano wa kubadili mahali zinakofanyikia na pia kutohudhuria mahali ambapo sherehe husika zinafanyika. Hali hiyo imewashtua baadhi ya viongozi wa zamani na wa sasa kitaifa, na sasa wameliambia gazeti hili kwamba ni muhimu zitungwe sheria za kuhakikisha matukio hayo yanaadhimishwa kwa wakati wake, namna yake na mahali pake kila mara.
Wakizungumza na muadishi wetu Ambapo kwa sababu za wazi hatuwezi kutaja majina ya viongozi iliozungumza nao, wamesema kwamba matamshi ya wiki iliyopita ya Magufuli wakati akiwa ziarani kwenye mikoa ya Kanda ya Ziwa "yamewashtua".
Akiwa katika ziara yake mkoani Shinyanga, Rais Magufuli alihutubia wakazi wa mkoa huo katika siku ambayo maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar yalikuwa yakiendelea katika Uwanja wa Abeid Aman Karume mjini Zanzibar.
Katika hotuba yake, pamoja na mambo mengine, Rais alisema maadhimisho ya Mapinduzi ya Zanzibar yanaweza kufanyika popote nchini, ikiwamo Tanzania Bara, katika dhamira ya kuhakikisha jambo hilo haliwi la Wazanzibari pekee bali Watanzania wote kwa ujumla.
Kiongozi mmoja mstaafu, kutoka Tanzania Bara, amelieleza kwamba mjadala wa kitaifa kuhusu namna ya kuadhimisha sherehe zinazoashiria asili ya taifa la Watanzania hauepukiki wakati huu kwa kuwa viongozi wa kitaifa sasa wameonyesha kutoheshimu mila na desturi za taifa.
Mwanasiasa huyo alisema kuwa mwisho wa mjadala huu ni kutunga sheria za kuwabana viongozi wakuu waliopo ama watakaoingia madarakani baadaye, wafuate sheria utaratibu uliowekwa na waasisi.
"Jambo hili, la kuweka utaratibu rasmi wa kisheria au wa kikatiba, ni muhimu sasa hasa ikizingatiwa kuwa taifa hili sasa ni la mfumo wa vyama vingi na chama chochote cha siasa kinaweza kuingia madarakani.
“Tumesikia kuna viongozi wakubwa katika baadhi ya vyama vya siasa hawataki kukubaliana na Muungano, tena wengine wakitoa kauli za kuashiria kuuvunja au kuudhoofisha kabisa. Hawa ni lazima wabanwe kikatiba si tena kwa mujibu wa mila na desturi za taifa,” alisema kiongozi huyo mstaafu.
Viongozi waliozungumza na gazeti hili pia hawakubaliani na suala la kubadilisha mahali pa kuadhimisha Siku ya Uhuru wa Tanganyika, wakieleza kwamba Uwanja wa Uhuru una historia yake katika jambo la Watanganyika kujitawala wenyewe.
@Raimwema