- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
News: Jaji mkuu alie teuliwa na Trump AMGEUKA asema "Trump lazima afate sheria"
Washington Marekani: Hivi karibuni kumekuwa na vitendo vya kutunishiana misuli kati ya Rais wa Marekani Bw Donald Trump na Majaji wa mahakama za nchi hiyo hasa baada ya Trump kuweka zuio la muda la kutaka Raia kutoka nchi saba zenye idadi kubwa ya Waislam kuzuiwa kuingia nchini marekani, sasa Jana kwenye kikao cha maseneta Jaji aliyependekezwa na Rais wa Marekani Donald Trump kujaza nafasi iliyo wazi katika Mahakama ya Juu nchini humo Bw Neil Gorsuch, amesema hakuna mtu yeyote aliye juu ya sheria, hata Rais Trump aliyependekeza uteuzi wake.
Gorsuch ameambia kikao cha bunge la Seneti kwamba hakuna mtu yeyote aliyemtaka kutoa ahadi kuhusu jinsi atakavyofanya maamuzi yake pindi atakapoidhinishwa kuwa jaji katika mahakama hiyo.
Pia Amesema angekataa uteuzi huo iwapo Bw Trump angemtaka kubatilisha uamuzi wa kihistoria wa mahakama katika kesi Roe v Wade ambao ulihalalisha utoaji wa mimba. Bw Gorsuch pia alishutumu vikali hatua ya Trump kuwashambulia kwa maneno majaji wa mahakama mara kwa mara na kusema "inavunja moyo".
Februari, rais huyo alimweleza jaji aliyebatilisha marufuku yake ya usafiri dhidi ya raia wa nchi saba kama "mtu huyo anayeitwa jaji".
Msemaji wa ikulu ya White House Sean Spicer baadaye aliandika kwenye Twitjer kwamba Bw Gorsuch alikuwa akizungumza "kwa mapana" na kwamba hakumtaja mtu kwa jina." Wakati wa kikao chake cha kwanza kuhojiwa na maseneta, Gorsuch, ambaye ni jaji wa Colorado aliulizwa maswali mengi kuhusu msimamo wake.
Maseneta wa Democrat walisisitiza kuhusu baadhi ya mambo yenye utata, lakini alisisitiza mara kwa mara kwamba ingekuwa makosa kwake kueleza angetoa uamuzi wa aina gani katika kesi yoyote hilo.