Home | Terms & Conditions | Help

November 29, 2024, 11:28 am

NEWS: JAJI MKUU AKUTANA NA TLS KUJADILI UTOAJI HAKI NCHINI

Dar es salaam: Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Profesa Ibrahimu Juma amekutana na kufanya mazungumzo na Chama cha mawakili Tanzania TLS wakiongozwa na Rais wake Fatma Karume na kuelezwa mpango mkakati ambao ndiyo dira ya mahakama kwa sasa.

Fatma karume na Jaji mkuu. Picha Mtanzania

Uongozi huo wa TLS umekutana na Jaji Mkuu na wadau wengine wa mahakama leo Jumanne Julai 24, ambapo Msajili Mkuu wa Mahakama, Catherine Revocati pamoja na mambo mengine amesema hiyo ni fursa ya kuanza kushirikiana.

“Mpango mkakati ndiyo dira ya mahakama, tunaomba ushirikiano katika eneo la Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama), lazima tubadilike, twende dunia inavyokwenda, tuachane na matumizi ya karatasi.

“Mawakili ni wadau wetu muhimu, bila wao sisi hatuwezi kufanya kazi, na wao bila sisi hawawezi kufanya kazi, tulianza nao, wameanza kujiandikisha katika mfumo mpya, tunaomba muendelee kutupigia debe waendelee kujiandikisha,” amesema Revocati.

Kwa upande wake Rais wa TLS, Fatma amesema mahakama haiwezi kuboresha mazingira ya utoaji haki katika maamuzi kama hawatazungumza na TLS.