November 29, 2024, 11:59 pm
- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: IDARA YA UHAMIAJI YATOA VIBALI MAALUMU KWA WAHAMIAJI TOKA BURUNDI
KIGOMA: Idara ya Uhamiaji nchini imeweka utaratibu wa kutoa kibali maalum kwa raia wa Burundi ambao wanataka kuja nchini kwa ajili ya kufanya shughuli za kilimo ikiwa ni moja ya nia za kupunguza raia wa nchi hiyo ambao huingia nchini kinyemela hususani katika mikoa ya Kigoma na Tabora kwa ajili ya kufanya kazi za kilimo kama vibarua.
Mpango huo umetangazwa na Kamishna Jenerali wa uhamiaji nchini Dk.Anna Makakala mwishoni mwa ziara yake iliyomfikisha katika wilaya zote na katika maeneo ya mpaka na nchi jirani mkoani Kigoma ambapo amesema vibali hivyo vya miezi mitatu vitawezesha raia hao kutambuliwa na serikali kupata fedha na kutambua wako wapi na idadi yao.Kwa upande wao baadhi ya wananchi wamesema uamuzi huo wa idara ya uhamiaji utasadia kupunguza uhalifu na kuongeza tija katika kilimo pamoja na kujenga mahusiano mazuri na nchi jirani ya burundi ambayo raia wake wanaongoza kwa kuja nchini kufanya vibarua bila ya kibali na hivyo kuongeza idadi ya wahamiaji haramu.
Newest Posts